6
1 Basi kwa mara nyingine Daudi akawakusanya wateuli wa Israeli, elfu thelathini.
2 Daudi akainuka na akaenda na watu wake wote waliokuwa pamoja naye kutoka Baala ulioko Yuda ili alilete sanduku la Mungu, liitwalo kwa jina la Yahwe wa majeshi, akaaye juu ya makerubi.
3 Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wanawe, wakauongoza mkokoteni.
4 Wakautoa mkokoteni na sanduku la Mungu juu yake nyumbani mwa Abinadabu juu ya kilima. Ahio alikuwa ametangulia mbele ya sanduku.
5 Kisha Daudi na nyumba yote ya Israeli wakaanza kucheza mbele ya Yahwe, wakishangilia kwa vyombo vya mziki, vinubi, vinanda, matari, kayamba na matowazi.
6 Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia.
7 Kisha asira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.
8 Daudi akakasirika kwa kuwa Yahwe alimpiga Uza, naye akapaita mahali pale Peresi Uza. Eneo hilo linaitwa Peres Uza hata leo.
9 Daudi akamwogopa Yahweh siku hiyo. Akasema, “Sanduku la Yahwe lawezaje kuja kwangu?”
10 Hivyo Daudi hakuwatayari tena kulichukua sanduku la Yahwe katika mji wa Daudi. Badala yake, akaliweka kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.
11 Sanduku la Yahwe likakaa katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti kwa miezi mitatu. Kwa hiyo Yahwe akambariki yeye na nyumba yake yote.
12 Kisha mfalme Daudi akaambiwa, “Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.” Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.
13 Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.
14 Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.
15 Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.
16 Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamwona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.
17 Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.
18 Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.
19 Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.
20 Kisha Daudi akarudi ili aibariki familia yake. Mikali, binti Sauli, akatoka ili akutane na Daudi naye akasema, “Jinsi gani mtukufu mfalme wa Israeli alivyokuwa leo, aliyejiacha uchi mbele ya macho ya vijakazi miongoni mwa watumishi wake, kama mmoja wa wapumbavu ambaye bila aibu hujifunua yeye mwenyewe!”
21 Daudi akamjibu Mikali, “Nilifanya hivyo mbele ya Yahwe, aliyenichagua juu ya baba yako na juu ya familia yake yote, aliyeniweka kuwa kiongozi juu ya watu wa Yahwe, juu ya Israeli. Mbele ya Yahwe nitafurahi!
22 Nitakuwa nisiye na heshima hata zaidi ya hapa, na nitajishusha mbele za macho yangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliowasema, nitaheshimiwa.”
23 Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watato hata alipokufa.