2
1 Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye
2 Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
3 Kama mti wa mpera ulivyo miongoni mwa miti ya misituni, ndivyo mpenzi wangu alivyo miongoni mwa wanaume. Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana, na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu.
4 Amenileta kwenye ukumbi wa maakuli, na bendera yake juu yangu ilikuwa upendo. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
5 Ni uishe kwa keki za mizabibu na kuniuisha na mapera, kwa kuwa nimedhohofika na mapenzi. Mwanamke akizungumza mwenyewe
6 Mkono wake wakushuto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
7 Ninataka muhaidi, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtavuruga mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
8 Sauti ya mpenzi wangu hiyo! O, huyu yuwaja, akiruka ruka juu milima, akiruka vilimani.
9 Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
10 Mpenzi wangu alizungumza na mimi na kusema, “Amka, mpenzi wangu; mzuri wangu, twende pamoja nami.
11 Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kwenda.
12 Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu.
13 Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imestawi; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
14 Hua wangu, katika miamba ya mawe, katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima, acha nione uso wako. Acha nisikie sauti yako, kwa kuwa sauti ni tamu, na uso wako ni mzuri.” Mwanamke akiongea mwenyewe
15 Wakamate mbweha kwa ajili yetu, mbweha wadogo wanao haribu shamba za mizabibu, kwa kuwa shamba la mizabibu limestawi.
16 Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
17 Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima mawe mengi.