4
1 O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma kitamba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likienda chini kutoka Mlima Gileadi.
2 Meno yako ni kama kondoo walio nyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna ata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
3 Mdomo wako ni kama uzi mwekendu; mdo wako wapendeza. Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kitambaa chako cha uso.
4 Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
5 Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.
6 Hadi jioni ifike na vivuli viondoke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
7 Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
8 Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya Amana, kutoka juu ya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, kutoka mashimo ya milima ya chuwi.
9 Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo mmoja tu wako kwangu, kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
10 Jinisi gani upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo, na arufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote.
11 Midomo yako, bibi arusi wangu, yatiririka asali; asali na maziwa vichini ya ulimi wako; arufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.
12 Dada yangu, bibi arusi wangu ni bustani ilio fungwa, bustani ilio fungwa, chemchemi iliyo fungwa kwa muhuri.
13 Matawi yako ni kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti, na ya mimea ya hina na nardo,
14 Nardo na Zafarani, mchai na mdalasini pamoja na aina zote za uvumba, manemane na udi na aina tofauti za manukato.
15 Wewe ni bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayo shuka kutoka Lebanoni. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
16 Amka, upepo wa kaskazini; njoo, upepo wa kusini; vuma katika bustani yangu ili manukato yake yatoe marashi. Mpenzi wangu na aje katika bustani yake na kula matunda ya chaguo lake.