3
1 Kisha Yahwe akanionesha Yoshua kuhani mkuu amesimama mbele za malaika wa Yahwe na Shetani amesimama mkono wake wa kushoto kumshitaki kwa ajili ya dhambi.
2 Malaika wa Yahwe akamwambia Shetani, “Yahwe na akukemee, Yahwe, aliyeuchagua Yerusalemu, akukemee! Je hiki si kinga kilichotolewa motoni”
3 Yoshua alikuwa na mavazi machafu aliposimama mbele ya malaika.
4 Malaika akawaambia waliosimama mbele yake, “Mvulisheni hayo mavazi machafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama! nimeuondoa uovu wako na nitakuvika mavazi safi.”
5 Haya wamvike kilemba safi kichwani!” Hivyo wakaweka kilemba safi kichwani pa Yoshua na wakamvika mavazi safi wakati malaika wa Yahwe amesimama kando.
6 Kisha malaika wa Yahwe akamwagiza Yoshua na kusema,
7 Yahwe wa majeshi asema hivi: “Ikiwa utatembea katika njia zangu, na kutunza amri zangu, ndipo utakapoisimamia nyumba yangu na kulinda nyua zangu, kwa maana nitakuruhusu kwenda na kutoka kati ya wasimamao mbele zangu.
8 WeweYoshua kuhani mkuu na wenzako wanaoishi nawe! Sikilizeni. Watu hawa ni ishara, kwa kuwa mimi mwenyewe nitamwinua mtumishi wangu aitwaye Tawi.
9 Tazameni jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua. Kuna macho saba juu ya jiwe hili moja, nami nitaandika maneno juu yake - asema Yahwe wa majeshi - nami nitaondoa dhambi katika nchi hii kwa siku moja.
10 Katika siku hiyo kila mtu atamwalika jirani yake kukaa chini ya mzabibu na mtini wake.” asema Yahwe wa majeshi.