Zaburi 100
Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu
Zaburi ya shukrani.
Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
Mwabuduni Bwana kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
 
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Kwa maana Bwana ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.