Zaburi 117
Sifa Za Bwana
Msifuni Bwana, enyi mataifa yote;
mtukuzeni yeye, enyi watu wote.
Kwa kuwa upendo wake kwetu ni mkuu,
uaminifu wa Bwana unadumu milele.
 
Msifuni Bwana.