8
Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. siku hiyo ndipo alipoanza kuwatesa kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote waliotawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume. Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake. Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwaburuza nje wanawake na waume, na kuwatupia gerezani. waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walilihubiri neno. Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko. Baada ya makutano kusikia na kuona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichosema. Kutoka hapo watu wengi waliosikia, pepo wachafu waliwatoka watu huku wakilia kwa sauti kubwa, na wengi waliopooza na viwete waliponywa. Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji. Lakini palikuwa na mtu mmoja katika mji ule jina lake Simon, ambaye alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa taifa la Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu. 10 Wasamaria wote tangu mdogo hata mkubwa, wakamsikiliza; wakasema;”mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu.” 11 Wakamsikiliza, kwa maana amewashangaza muda mrefu kwa uchawi wake. 12 Lakini wakati walipoamini kuwa Filipo alihubiri juu ya ufalme wa Mungu na juu ya jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanaume kwa wanawake. 13 Na Simoni mwenyewe aliamini: baada ya kubatizwa, aliendelea kuwa na Filipo; alipoona ishara na miujiza iliyokuwa ikitendeka, alishangaa. 14 Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma Petro na Yohana. 15 Wakati walipokuwa wakishuka wakawaombea; kwamba wampokee Roho Mtakatifu. 16 Mpaka muda huo, Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 17 Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu. 18 Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa, 19 Akasema, “Nipeni hii nguvu, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.” 20 Lakini Petro akamwambia; pesa yako pamoja na wewe ipotelee mbali, kwa sababu umedhani kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa. 21 Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu. 22 Hivyo basi tubu maovu yako na kumwomba Mungu labda utasamehewe fikra za moyo wako. 23 Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi.” 24 Simoni akajibu na kusema, “Mwombeni Bwana kwa ajili yangu, kwa kuwa mambo yote mliyozungumza yaweza kunitokea. 25 Wakati Petro na Yohana walipokuwa wameshuhudia na kuhubiri neno la Bwana, walirudi Yerusalemu kwa njia hiyo; walihubiri injili katika vijiji vingi vya Wasamaria. 26 Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Angaza na uende kusini katika njia iendayo chini ya Yerusalemu kuelekea Gaza.” ( Njia hii iko katika jangwa). 27 Akaangaza na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya kandase; malkia wa Ethiopia. Aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu. 28 Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo. 30 “Hivyo Filipo akaenda mbio, akamsikia akisoma katika chuo cha nabii Isaya; akasema, Je unafahamu unachosoma?” 31 Muethiopia akasema, “nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye. 32 Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa; na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake: 33 Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? maisha yake yameondolewa katika nchi.” 34 Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine”?. 35 Filipo alianza kuongea, alianza kwa andiko hili la Isaya kumhubiria habari za Yesu. 36 Wakiwa njiani, wakafika penye maji,' towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa nini kinazuia nisibatizwe?, 37 maneno haya, “Hivyo Muethiopia akajibu “naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu,” hayamo kwenyemaandiko ya kale). Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame. 38 Walikwenda ndani ya maji, pamoja Filipo na towashi, Filipo akambatiza. 39 Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana ikampeleka Filipo mbali; towashi hakumwona, akaenda njia yake akishangilia. 40 Lakini Philipo akatokea Azoto. Alipita katika mkoa ule na kuhubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.