19
Ndipo Ayubu akajibu na kusema, lini mtanifanya mimi kuteseka na kunivunja vunja mimi vipande vipnde kwa maneno? Mara kumi hivi mmenishutumu mimi; ninyi hamuoni aibu kwamba mmenitendea mimi kwa ukatili. Kama ni dhahiri kweli mimi nimekosa, makosa yangu hubaki kuwa wajibu wangu. Kama ni dhahiri ninyi mtajiinua juu yangu mimi na kuutumia uvumilivu wangu kunipinga mimi, kisha ninyi mnapaswa kutambua kwamba Mungu amefanya mabaya kwangu mimi na amenikamata mimi katika mtego wake yeye. Tazama, Mimi ninalia kwa sauti, “dhuluma!” lakini sipati jibu. Mimi ninaita kwa ajili ya msaada, lakini hakuna haki. Yeye ameiwekea ukuta njia yangu, ili kwamba mimi nisiweze kupita, na yeye ameweka giza katika njia yangu. Yeye ameniondoa Mimi kutoka katika utukufu wangu, na ameichukua taji kutoka kwenye kichwa changu mimi. 10 Yeye amenivunjavunja mimi chini kwa kila upande, na Mimi nimetoweka; yeye amelikokota juu tumaini langu kama mti. 11 Yeye pia ameiongeza ghadhabu yake dhidi yangu mimi; yeye ananihesabu mimi kama mmoja wa adui zake. 12 Majeshi yake huja juu pamoja; wao wananikosesha tumaini kwa kuniteka nyara kwa kundi kubwa kupigana na mimi wakizunguka hema yangu. 13 Yeye amewaweka ndugu zangu mbali kutoka kwangu mimi; watu wangu wa karibu wote wamejitenga kutoka kwangu mimi. 14 Vizazi vyangu vimeniangusha mimi; rafiki zangu wa karibu wamenisahamu mimi. 15 Wale ambao mwanzoni walikaa kama wageni ndani ya nyumba yangu na watumishi wangu wa kike, hunihesabu mimi kama mgeni. Mimi nimekuwa mgeni katika macho yao. 16 Mimi ninamwita mtumishi wangu, lakini yeye hanipi jibu japokuwa Mimi nimemsihi yeye kwa midomo yangu. 17 Pumzi yangu mimi ni chukizo kwa mke wangu; Hata mimi ninachukiwa na wale ambao walizaliwa kutoka katika tumbo la mama yangu mimi. 18 Hata watoto wachanga wananichukia mimi; ikiwa Mimi nitainuka kuzungumza, wao huzungumza dhidi yangu mimi. 19 Rafiki zangu wote ninaowazoea wananichukia sana mimi; wale ambao Mimi ninawapenda wamegeuka kinyume na mimi. 20 Mifupa yangu inashikamana kwenye ngozi yangu na kwenye mwili wangu; Mimi ninaishi tu kwa ngozi ya meno yangu. 21 Iweni na huruma juu yangu mimi, muwe na huruma juu yangu mimi, rafiki zangu, kwa maana mkono wa Mungu umenigusa mimi. 22 Kwa nini mnanitesa mimi kama ninyi mlikuwa Mungu? kwa nini hamjatosheka bado kwa kula mwili wangu? 23 Laiti, hayo maneno yangu yangekuwa yameandikwa chini! Laiti, hayo yangekuwa yameandikwa katika kitabu! 24 Laiti, kwa kalamu ya chuma na risasi hayo yangekuwa yamechorwa katika mwamba siku zote! 25 Lakini kama ilivyo kwangu mimi, Mimi ninafahamu kwamba mkombozi wangu anaishi, na kwamba hata mwisho atasimama katika nchi; 26 baada ya ngozi yangu, hivyo ndivyo, mwili huu, unaharibiwa, ndipo katika mwili wangu mimi Nitamwona Mungu. 27 Mimi nitamwona yeye kwa macho yangu mwenyewe-Mimi, na siyo mtu mwingine. Moyo wangu hushindwa ndani yangu mimi. 28 Kama mnatasema, 'Kwa jinsi gani tutamtesa yeye? Mzizi wa mahangaiko yake unakaa katika yeye; 29 ndipo uwe umeogopeshwa kwa ule upanga, kwa sababu ghadhabu huleta hukumu ya upanga, hivyo kwamba wewe uweze kutambua kuna hukumu.”