20
1 Ndipo Sofari, Mnaamathi alijibu na kusema,
2 “Mawazo yangu yananifanya mimi nijibu kwa haraka kwa sababu ya mashaka yaliyomo ndani yangu mimi.
3 Mimi ninasikia kukemewa ambako kunaniondolea heshima mimi, lakini roho kutoka katika ufahamu wangu hunijibu mimi.
4 Je, unafahamu kwamba ukweli huu kutoka enzi za kale, wakati Mungu alipomweka mwanadamu juu ya nchi:
5 ushindi wa mtu mwovu ni mfupi, na furaha ya mtu asiyemcha Mungu hudumu kwa kitambo tu?
6 Ingawa urefu wake yeye hufikia juu kwenye mbingu, na kichwa chake yeye kufikia kwenye mawingu,
7 bado mtu huyo atapotea siku zote kama mavi yake yeye mwenyewe; wale waliokuwa wamemuona yeye watasema, 'Yuko wapi yeye'?
8 Yeye atapaa mbali kama ndoto na hataonekana; ndivyo ilivyo, yeye atakuwa amefukuzwa mbali kama ono la
9 usiku. Jicho ambalo lilimuona yeye halitamuona yeye tena; mahali pake hapatamuona yeye tena.
10 Watoto wake wataomba msamaha kwa watu maskini, mikono yake itaweza kurudisha utajiri wake.
11 Mifupa yake imejaa nguvu za ujanani, lakini zitalala naye chini katika mavumbi.
12 Japokuwa uovu ni mtamu katika mdomo wake yeye, japokuwa yeye anauficha chini ya ulimi wake yeye,
13 japokuwa anaushikilia pale na hauruhusu kwenda lakini bado huushikilia katika mdomo wake yeye -
14 chakula katika koromeo lake yeye hugeuka kuwa uchungu; hugeuka kuwa sumu ya majoka ndani yake yeye.
15 Yeye humeza chini utajiri, lakini yeye atautapika tena; Mungu atautoa nje kutoka katika tumbo lake yeye.
16 Yeye atamumunya sumu ya majoka; ulimi wa nyoka mwenye sumu utamwua yeye.
17 Yeye hatafurahia vijito vya maji, wingi wa asali na siagi.
18 Yeye atayarudisha matunda ya kazi yake na hataweza kuyala; yeye hatafurahia utajiri alioupata kwa biashara zake yeye.
19 Kwa kuwa yeye amewakandamiza na kuwasahau watu maskini; yeye kwa uonevu, amezichukua mbali nyumba ambazo hakuzijenga yeye.
20 Kwa sababu yeye mwenyewe hakujua utoshelevu wowote, yeye hataweza kuokoa kitu chochote katika kile ambacho alijifurahisha.
21 Hakuna chochote kilichoachwa ambacho yeye hakukimeza; kwa hiyo mafanikio yake yeye hayatakuwa ya kudumu.
22 katika wingi wa utajiri wake yeye ataanguka katika mahangaiko; mkono wa kila mmoja ambaye yuko katika umaskini utakuja kinyume chake yeye.
23 Wakati akiwa katika kulijaza tumbo lake, Mungu atatupa hasira ya ghadhabu yake juu yake yeye; Mungu ataunyeshea chini juu yake yeye wakati yeye anakula.
24 Ingawa mtu huyo atakimbia kutoka katika silaha ya chuma, upinde wa shaba utampiga yeye.
25 Mshale utatoboa kupitia mgongoni mwake na utatokezea; ni dhahiri, ncha inayong'ra itatokezea nje kupitia ini lake yeye; watesi huja tena juu yake.
26 Giza lliilo kamilika limetunzwa kwa akiba zake; moto usiopulizwa utamla yeye kwa haraka; utameza kile kilichoachwa katika hema yake.
27 Mbingu zitauweka wazi uovu wake, na nchi itainuka juu dhidi yake yeye kama shahidi.
28 Utajiri wa nyumba yake utatoweka; bidhaa zake zitamwagika mbali siku ya ghadhabu ya Mungu.
29 Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kutoka kwa Mungu, urithi uliotunzwa akiba na Mungu kwa ajili yake yeye.”