11
1 Hili ndilo neno lililojia Yeremia kutoka kwa Bwana, akasema,
2 “Sikiliza maneno ya agano hili, uwaambie kila mtu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
3 Uwaambie, 'Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: na alaaniwe yeyote asiyesikiliza maneno ya agano hili.
4 Hili ndilo agano nililowaamuru baba zenu walishike siku nilipowatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka tanuru ya chuma. Nikawaambia, “Sikilizeni sauti yangu na mfanye mambo yote kama nilivyowaamuru, kwa kuwa mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.”
5 Nisikilizeni ili nipate kukitimiza kiapo nilichoapa kwa baba zenu, kiapo kwamba nitawapa nchi iliyojaa maziwa na asali kama ilivyo leo.'” Kisha mimi Yeremia nikajibu na kusema, “Ndio, Bwana!”
6 Bwana akaniambia, “Hubiri habari hizi yote katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu. Sema, “Sikilizeni maneno ya agano hili na mkayafanye.
7 Kwa maana nimewaagiza wazee wenu tangu siku ile niliyowaleta kutoka nchi ya Misri hadi wakati huu wa sasa, nimewaonya mara kwa mara na kusema, “Sikilizeni sauti yangu.'”
8 Lakini hawakusikiliza au wala kutega masikio yao. Kila mtu amekuwa akitembea katika ukaidi wa moyo wake mbaya. Kwa hiyo nilileta laana zote katika agano hili nililoamuru kuja juu yao. Lakini watu bado hawakuitii.”
9 Kisha Bwana akaniambia, “Njama imeonekana kati ya watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.
10 Wameugeukia uovu wa mababu zao wa mwanzo, ambao walikataa kusikiliza neno langu, ambao badala yake walifuata miungu mingine ili kuabudu. Waisraeli na nyumba ya Yuda walivunja agano langu nililoweka na baba zao.
11 Kwa hiyo Bwana asema hivi, 'Tazameni, nitawaletea majanga juu yao, majanga ambayo hawataweza kuyaepuka. Ndipo wataniita, lakini sitawasikiliza.
12 Miji ya Yuda na wenyeji wa Yerusalemu watakwenda na kuiita miungu ambayo walitoa sadaka, lakini hakika hawatawaokoa wakati wa majanga yao.
13 Kwa kuwa idadi ya miungu yako ewe Yuda imeongezeka sawa na idadi ya miji yako. Na umefanya idadi ya madhabahu ya aibu huko Yerusalemu, madhabahu ya kufukiza uvumba kwa Baali, sawa na idadi ya njia zake.
14 Kwa hiyo wewe mwenyewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa. Lazima usiomboleze au kuomba kwa niaba yao. Kwa maana siwezi kusikiliza wakati wananiita katika majanga yao.
15 Mpendwa wangu anafanya nini nyumbani kwangu, ikiwa amekuwa na nia mbaya? Nyama za sadaka yako hazitakusaidia. Unafurahi kwa sababu ya matendo yako mabaya.
16 Katika siku za nyuma Bwana alikuita mti wa mzeituni wenye majani, mzuri wenye matunda mazuri. Lakini atawasha moto juu yake ambayo itaonekana kama sauti ya dhoruba; matawi yake yatavunjika.
17 Kwa maana Bwana wa majeshi, aliyekua amekusudia maafa juu yako, kwa sababu ya matendo mabaya ambayo nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamefanya-wamenikasirisha kwa kumtolea Baali sadaka.'”
18 Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nakayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao.
19 Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, “Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena.
20 Lakini Bwana wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.
21 Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya watu wa Anathothi, wanaotafuta uhai wako, “wanasema, 'Usifanye unabii kwa jina la Bwana, usije utakufa kwa mkono wetu.'
22 Kwa hiyo Bwana wa majeshi asema hivi, 'Tazameni, nitawaadhibu. Vijana wao wenye nguvu watakufa kwa upanga. Wana wao na binti zao watakufa kwa njaa.
23 Hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa maana nitaleta maafa dhidi ya watu wa Anathothi, mwaka wa adhabu yao.'”