12
1 Wewe ni mwenye haki, Bwana, wakati wowote ninapoleta mashitaka kwako. Lazima nikuambie sababu yangu ya kulalamika: Kwa nini njia za waovu hufanikiwa? Watu wote wasiokuwa na imani wanafanikiwa.
2 Wewe uliwapanda nao wakawa na mizizi. Wanaendelea kuzaa matunda. Wewe upo karibu nao katika vinywa vyao, lakini mbali na mioyo yao.
3 Lakini wewe mwenyewe unanijua, Bwana. Umeona mimi na kuchunguza moyo wangu. Waondoe kama kondoo wa kuchinjwa. Ukakaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
4 Je! Nchi itakauka kwa muda gani, na mimea katika kila shamba itaota kwa sababu ya uovu wa wenyeji wake? Wanyama na ndege wameondolewa. Hakika, watu wanasema, “Mungu hajui nini kitatokea kwetu.”
5 Bwana akasema, “Kweli, wewe, Yeremia, umetembea na askari wa miguu na wamechoka, unawezaje kushindana dhidi ya farasi? Ikiwa unashuka chini ya nchi iliyo salama, utafanyaje katika misitu karibu na Yordani?
6 Kwa maana hata ndugu zako na familia ya baba yako wamekudharau na kukukemea kwa sauti kubwa. Usiwaamini, hata kama wanasema mambo mazuri kwako.
7 Nimeiacha nyumba yangu; Nimeacha urithi wangu. Nimewatia watu wangu wapendwa mikononi mwa adui zake.
8 Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba katika tundu; yeye hujiweka juu yangu kwa sauti yake mwenyewe, hivyo nimemchukia.
9 Malipo yangu ya thamani ni fisi, na ndege wenye madoadoa karibu na kichwa chake. Nenda, ukakusanye viumbe vyote vilivyomo katika mashamba, na uwalete ili wale.
10 Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu. Wameipoteza sehemu yangu yote ya ardhi; Waligeuza sehemu yangu nzuri kuwa jangwa, ukiwa.
11 Wamemfanya kuwa ukiwa. Ninaomboleza kwa ajili yake; yeye ni ukiwa. Nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa maana hakuna mtu aliyeweka haya moyoni mwake.
12 Waangamizi wamekuja juu ya maeneo yote yaliyo wazi jangwani, kwa maana upanga wa Bwana unakula kutoka upande mmoja wa nchi hadi mwingine. Hakuna usalama katika nchi kwa kiumbe chochote kilicho hai.
13 Walipanda ngano lakini mavuno ya miiba. Wao wamechoka kutokana na kazi lakini hawajapata chochote. Basi muaibike kwa faida yenu kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana.”
14 Bwana asema hivi dhidi ya majirani zangu wote, waovu wanaopiga milki niliyowarithisha watu wangu Israeli, “Tazama, mimi ndimi ambaye nitawafukuza kutoka nchi yao wenyewe, nami nitaifuta nyumba ya Yuda kutoka kati yao.
15 Ndipo baada ya kuangamiza mataifa hayo, itatokea kwamba nitakuwa na huruma juu yao na kuwaleta tena; Nitawarudi-kila mtu kwa urithi wake na nchi yake.
16 Kisha itakuwa ikiwa mataifa hayo yatajifunza kwa makini njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu 'Kama Bwana anaishivyo!' vile vile kama walivyowafundishwa watu wangu kuapa kwa Baali, basi watajengwa katikati ya watu wangu.
17 Lakini kama hakuna yeyote anayesikiliza, basi nitaling'oa taifa hilo. Kwa hakika litang'olewa na kuharibiwa-hili ndilo tamko la Bwana.”