29
1 Haya ni maneno katika waraka ambao Yeremia nabii alituma kutoka Yerusalemu kwa wazee waliosalia miongoni mwa mateka na makuhuni, manabii, na watu wote ambao Nebukadreza aliwapeleka utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli.
2 Hii ilikuwa baada ya Yekonia mfalme, mama yake mfalme, na watumishi wakuu, viongozi wa Yuda na Yerusalemu, na wahunzi walikuwa wamepelekwa mbali na Yerusalemu.
3 Aliutuma waraka huu kwa mkono wa Elasa mwana wa Shafani, Gemaria, mwana wa Hilkia, ambaye Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemtuma kwa Nebukadreza mfalme wa Babeli
4 Waraka ulisema, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kwa mateka ambao niliwasababisha kuwa mateka kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
5 'Jengeni nyumba na muishi ndani yake. Pandeni bustani na mle matunda yake.
6 Chukueni wake na mzae wana na mabinti. Kisha Kisha chukueni wake kwa ajili ya wana wenu, na wapatieni waume binti zenu. Wazae wana na mabinti na waongezeke ili msiwe wachache sana.
7 Itafuteni amani ya mji ambako nimewafanya kuwa watumwa, na mkauombee kwangu kwa niaba yake kwa kuwa kutakuwa na amani kwenu kama mji uko katika amani.'
8 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, 'Msiwaache manabii ambao wako katikati yenu na wabashiri wenu kuwadanganya, na msizisikilize ndoto ambazo ninyi wenyewe mnaota.
9 Kwa maana wanatabiri uongo kwenu katika jina langu. Mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahwe.'
10 Kwa maana Yahwe anasema hivi, 'Babeli atakapokuwa amewatawala kwa muda wa mika sabini, nitawasaidia ninyi na kulitimiza neno langu jema kwa ajili yenu ili kuwarudisha ninyi katika sehemu hii.
11 Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipangao niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahwe—mipango kwa ajili ya amani na siyo kwa ajili ya mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini na siku zenu za mwisho.
12 Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza.
13 Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.
14 Kisha nitapatikana kwenu—hili ni tangazo la Yahwe—na nitawarudisha watu wenu waliofungwa; nitawakusanya kutoka mataifa yote na sehehemu zote ambako nimewatawanya—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitawarudisha kutoka sehemu ambako niliwasababisha kuwa mateka.
15 Tangu mliposema kwamba Yahwe ameinua manabii kwa ajili yetu katika Babeli,
16 Yahwe anasema hivi kwa mfalme aliyeketi katika kiti cha enzi cha Daudi na watu wote wakaao katika mji huo, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi utumwani—
17 Yahwe wa majeshi anasema hivi, ''Ona, niko karibu kutuma upanga, njaa, na ugonjwa juu yao. Kwa maana nitawafanya kuwa kama tini mbovu ambazo ni mbaya sana hazifai kuliwa.
18 Kisha nitawafuata kwa upanga, njaa, na tauni na kuwafanya kuwa kitu cha kushangaza kwa falme zote juu ya dunia—kitu cha kuogofya, kitu cha kulaaniwa na kuzomewa, na kitu cha aibu miongoni mwa mataifa yote ambako nilimtawanya.
19 Hii ni kwa sababu hawakulisikiliza neno langu—hili ni tangazo la Yahwe—ambalo nililituma kwao kupitia watumishi wangu manabii. Niliwatuma tena na tena, lakini hamkusikiliza—hili ni tangazo la Yahwe. '
20 Kwa hiyo ninyi wenyewe sikilizeni neno la Yahwe, ninyi mateka wote ambao amewatuma kutoka Yerusalemu hadi Babeli,
21 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya na Sedekia mwana wa Maaseya, watabirio uongo kwenu katika jina langu: Ona, niko karibu kuwaweka katika mkono wa Nebukadreza mfalme wa Babeli. Atawaua mbele ya macho yenu.
22 Kisha laana itatamkwa na wafungwa wote wa Yuda katika Babeli kuhusu watu hawa. Laana itasema: Yahwe awafanye kuwa kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka kwenye moto.
23 Hili litatokea kwa sababu ya mambo ya aibu waliyofanya katika Israeli walipofanya uzinzi na wake za majarani zao na kutangaza maneno ya uongo katika jina langu, mambo ambayo sikuwaamuru wayaseme. Kwa maana mimi ndiye nijuaye; mimi ni shahidi—hili ni tangazo la Yahwe.”'
24 Kuhusu Shemaya Mnehelami, sema hivi:
25 'Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwa sababu ulituma barua kwa jina lako kwa watu wote katika Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa Maaseya kuhani, na kwa makuhani wote, na ulisema,
26 “Yahwe aliwafanya ninyi kuwa makuhani badala ya Yehoyada kuhani, ili muwe wasimamizi wa nyumba ya Yahwe. Ninyi ni viongozi wa watu wote wajitiao wazimu na kujifanya wenyewe manabii. Mtawaweka katika mkatale na minyororo.
27 Kwa hiyo sasa, kwa nini hamkumkemea Yeremia wa Anathothi, ambaye hujifanya mwenyewe nabii juu yenu?
28 Kwa maana ametutumia sisi katika Babeli, 'Itakuwa muda mrefu. Jengeni nyumba na muishi ndani yake, na pandeni busitani na mule matunda yake.””
29 Sefania kuhani akaisoma barua hii mbele ya Yeremia nabii.
30 Kisha neno la Yahwe likaja kwa Yeremia, likisema,
31 “tuma neno kwa mateka wote na sema, 'Yahwe anasema hivi kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi wakati mimi sikumtuma, na amewaongoza kuamini uongo,
32 kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kumwadhibu Shemaya Mnehelami na uzao wake. Hapatakuwa na mtu wa kukaa miongoni mwa watu hawa kwa ajili yake. Hataona mema nitakayofanya kwa ajili ya watu wangu—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana ametangaza uasi dhidi ya Yahwe.””