28
Ilitokea katika mwaka ule, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne na mwezi wa tano, Hanania mwana wa Azuri nabii, alikuwa wa Gibeoni, alisema kwangu katika nyumba ya Yahwe mbele za makuhani na watu wote. Alisema, “Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeivunja nira iliyowekwa na mfalme wa Babeli. Ndani ya miaka miwili nitavirudisha katika sehemu hii vyombo vyote vya nyumba ya Yahwe ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli livichukua kutoka sehemu hii na kuvisafirisha hadi Babeli. Kisha nitawarudisha katika sehemu hii Yekonia mwana wa Yehotakimu, mfalme wa Yuda, na mateka wote wa Yuda ambao walipelekwa Babeli—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.” Kwa hiyo Yeremia nabii akasema kwa Hanania nabii mbele ya makuhani na kwa watu wote waliosimama katika nyumba ya Yahwe. Yeremia nabii akasema, “Yahwe afanye hivi! Yahwe ayathibitishe maneno ambayao ulitabiri na kuvirudisha katika sehemsu hii vyombo vya nyumb a ya Yahwe, na mateka wote kutoka Babeli. Vile vile, sikilizeni neno ambaloo ninalitangaza katika masikio yenu na katika masikio ya watu wote. Manabii ambao walikuwepo mbele yangu na na mbele yenu muda mrefu uliopita pia walitabiri kuhusu mataifa mengi na juu ya falme kuu, kuhusu vita, njaa, na mapigo. Kwa hiyo nabii anayetabiri kwamba kutakuwa na amani—kama neno lake litatimia, basi itajulikana kwamba yeye ni nabii kweli aliyetumwa na Yahwe.” 10 Lakini Hanania nabii akaichukua nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia na kuivunja. 11 Kisha Hanania akanena mbele ya watu wote na kusema, “Yahwe anasema hivi: Kama hivi tu, ndani ya miaka miwili nitaivunja nira iliyowekwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo ya kila taifa.” Kisha Yeremia nabii akaenda njia yake. 12 Baada ya Hanania nabii kuivunja nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia nabii, neno la Yahwe likamjia Yeremia. likisema, 13 Nenda na ukaseme kwa Hanania na useme, Yahwe anasema hivi: Uliivunja nira ya mbao, lakini badala yake nitafanya nira ya chuma.' 14 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma shingoni mwa mataifa haya yote ili wamtumikea Nebukadreza mfalme wa Babeli, na watamtumikia. Pia nimempa wanyama wa mashambani awatawale.” 15 Kisha nabii Yeremia akamwambia Hanania nabii, “Sikiliza Hanania! Yahwe hajakutuma, bali wewe mwenyewe umewasababisha watu hawa kuamini katika uongo. 16 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kukutuma nje ya dunia. Mwaka huu utakufa.” 17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, Hanania nabii akafa.