111
Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano. Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio. Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele. Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema. Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake. Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa. Kazi za mikono yake ni za kuaminika na haki; maagizo yake yote ni ya kuaminika. Yamethibitika milele, yamefanywa katika uaminifu na vizuri. Aliwapa ushindi watu wake; aliliteuwa agano lake milele; jina lake ni takatifu na lakutisha. 10 Kumcha Yahwe ni mwanzo wa hekima; wale washikao maagizo yake wana uelewa mzuri. Sifa yake yadumu milele.