115
1 Sio kwetu, Yahwe, sio kwetu, bali kwa jina lako ulete heshima, kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na uaminifu wako.
2 Kwa nini mataifa yalazimike kusema, “Yuko wapi Mungu wako?”
3 Mungu wetu aliye mbinguni; hufanya chochote apendacho.
4 Sanamu za mataifa ni fedha na dhahabu, kazi ya mikono ya wanadamu.
5 Sanamu hizo zina vinywa, lakini haziongei; zina macho, lakini hazioni;
6 zina masikio, lakini hazisikii; zina pua lakini hazinusi.
7 Sanamu hizo zina mikono, lakini hazishiki; zina miguu, lakini haziwezi kutembea; wala haziongei kutoka viywani mwao.
8 Wale wanao zitengeneza wanafanana nazo, vile vile yeyote anaye amini katika hizo.
9 Israeli, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
10 Nyumba ya Haruni, amini katika Yahwe; yeye ni msaada wako na ngao yako.
11 Ninyi mnao mheshumu Yahwe, mwamini yeye; yeye ni msaada wenu na ngao yenu.
12 Yahwe hutukumbuka sisi na atatubariki; ataibariki familia ya Israeli; atabariki familia ya Haruni.
13 Atawabariki wale wanao muheshimu yeye, wote vijana na wazee.
14 Yahwe na awaongeze ninyi zaidi na zaidi, ninyi pamoja na watoto wenu.
15 Yahwe na awabariki, aliyeziumba mbingu na nchi.
16 Mbingu ni za Yahwe; lakini nchi amewapa wanadamu.
17 Wafu hawamsifu Yahwe, wala wote washukao chini kwenye ukimya;
18 bali tutamtukuza Yahwe sasa na hata milele. Msifuni Yahwe.