12
Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye Sheminith. Zaburi ya Daudi. Msaada, Yahweh, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; nao waaminifu wametokomea. Kila mmoja anasema kwa jirani yake maneno matupu; kila mmoja anaongea kwa midomo yenye sifa za uongo na maneno ya udanganyifu. Yahweh, katilia mbali midomo yenye sifa za uongo, kila ulimi unanena kwa nguvu mambo makubwa. Hawa ni wale ambao wamesema, “Kwa ndimi zetu tutashinda. Wakati midomo yetu itakapo ongea, ni nani atakaye kuwa mtawala juu yetu?” “Kwa sababu ya vurugu zilizopo kinyume na maskini, na kwa sababu ya kuugua kwao wahitaji, Nitainuka,” asema Yahwe. “Nitawaletea usalama wanao hitaji.” Maneno ya Yahwe ni masafi, kama fedha iliyo safishwa katika tanuru duniani, iliyo ng'arishwa mara saba zaidi. Wewe ni Yahwe! Unaye watunza. Una wahifadhi wacha Mungu kutoka katika hiki kizazi cha waovu na hata milele. Waovu hutembea kila pande pale uovu unapoinuliwa kati ya wanadamu.