13
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mpaka lini, Yahweh, utaendelea kunisahau? Ni kwa muda gani utauficha uso wako nisiuone? Ni kwa muda gani nitalazimika kuhofu na kuhuzunika moyoni mwangu kila siku? Ni kwa muda gani adui zangu watanishida? Unitazame na unijibu, Yahwe Mungu wangu! Nipe mwanga machoni pangu, vinginevyo nitalala katika mauti. Usimuache adui yangu aseme, “Nimemshinda huyu,” ili kwamba asiweze kusema, “Nimemtawala adui yangu;” la sivyo, maadui zangu watafurahia nitakapo shushwa chini. Lakini nimeamini katika uaminifu wa agano lako; moyo wangu wafurahia katika wokovu wako. Nitamuimbia Yahwe kwa kuwa ameniganga kwa ukarimu kabisa.