120
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe, naye akanijibu. Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao. Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu? Atawaadhibu kwa mishale ya shujaa iliyo nolewa kwa makaa ya moto ya mretemu. Ole wangu mimi kwa sababu ninaishi kwa muda Mesheki; huko nyuma niliishi kati ya maskani ya Kedari. Kwa muda mrefu sana niliisha na wale waichukiao amani. Nipo kwa ajili ya amani, lakini ninenapo, wao wako kwa ajili ya vita.