126
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Bwana alipowarejesha mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto. Vinywa vyetu vilijawa na vicheko na ndimi zetu zilijawa na kuimba. Kisha wakasema kati ya mataifa, “Yahwe amewatendea mambo makuu.” Yahwe alitufanyia mambo makuu; ni furaha gani tuliyokuwa nayo! Ee Yahwe, uwarejeshe mateka wetu, kama vijito vya kusini. Wale wapandao kwa machozi watavuna kwa kelele za furaha. Yeye aendaye akilia, akibeba mbegu kwa ajili a kupanda, atarudi tena kwa kelele za furaha, akileta miganda yake.