125
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele. Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele. Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea. Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao. Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.