128
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu.
1 Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake.
2 Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa.
3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako.
4 Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa.
5 Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako.
6 Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli.