129
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia,” Israeli na iseme. “Mara nyingi tangu ujana wangu wamekuwa wakinishambulia, lakini hawajanishinda. Wakulima wamekuwa wakilima mgonngoni kwangu; wametengeneza matuta yao marefu. Yahwe ni mwenye haki; amezikata kamba za waovu.” Wote waaibishwe na kurudishwa nyuma, wale wachukiao Sayuni. Na wawe kama nyasi juu ya paa ambayo hunyauka kabla hayajakua, ambayo hayawezi kujaza mkono wa mvunaji wala kifua cha mfunga miganda. Wale wapitao karibu wasiseme, “Baraka za Mungu na ziwe juu yako; Tunakubariki katika jina la Yahwe.”