131
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu; wa Daudi. Yahwe, moyo wangu haujivuni wala macho yangu hayana kuburi. Sina matarajio makubwa kwa ajili yangu mwenyewe wala kujihofia kwa mambo ambayo yako juu ya uwezo wangu. Hakika nimejituliza na kuinyamazisha nafsi yangu; kama mtoto aliyeachishwa na mama yake, nafsi yangu ndani yangu iko kama mtoto aliye achishwa. Israeli, umtumainie Yahwe sasa na hata milele.