130
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Toka ndani yangu ninakulilia, Yahwe. Bwana, usikie sauti yangu; masikio yako na yasikie kwa makini kuomba kwangu kwa ajili ya huruma. Kama wewe, Yahwe, ungehesabu maovu, Bwana, ni nani angesimama? Lakini kwako kuna msamaha, ili uweze kuheshimiwa. Ninamngoja Yahwe, nafsi yangu inasubiri, na katika neno lake ninatumainia. Nafsi yangu inamngoja Bwana kuliko mlinzi aingojavyo asubuhi. Israeli, umtumainie yahwe. Yahwe ni wenye huruma, na yuko tayari kusamehe. Ni yeye ambaye ataikomboa istaeli dhidi ya dhambi zake zote.