137
Kando ya mito ya Babeli tuliketi na tulilia tulipokumbuka kuhusu Sayuni. Tulitundika vinubi vyetu kwenye miti ya Babylon. Huko watekaji wetu walitaka tuwaimbie, na wale walio tudhihaki walitutaka sisi tufurahi, wakisema, “Tuimbieni moja ya nyimbo za Sayuni.” Tungewezaje kuimba wimbo unaomuhusu Yahwe katika nchi ya ugeni? Kama nikikusahau wewe, Yerusalemu, basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake. Ulimi wangu na ushikamane juu ya kinywa changu kama nisipokufikiria tena, na kama sipendelei zaidi Yerusalemu kuliko furaha yangu kuu. Kumbuka, Ee Yahwe, kile walichofanya Waedomu siku ya anguko la Yerusalemu. Walisema, “Ibomoeni, ibomoeni mpaka chini kwenye misingi yake.” Binti za Babeli, hivi karibuni wataharibiwa- mtu na abalikiwe, yeyote atakaye walipizia yale mliotufanyia sisi. Mtu na abarikiwe, yeyote achukuaye na kusambaratisha watoto wenu juu ya jiwe.