149
Msifuni Yahwe. Mwimbieni Yahwe wimbo mpya; imbeni sifa zake katika kusanyiko la waaminifu. Israeli ishangilie katika yeye aliye iumba; watu wa Sayuni na washangilie katika mfalme wao. Nao walisifu jina lake kwa kucheza; na wamuimbie sifa yeye kwa ngoma na kinubi. Kwa kuwa Yahwe hupata furaha katika watu wake; huwapa utukufu wanyeyekevu kwa wokovu. Wacha Mungu wauchangilie ushindi; nao waimbe kwa furaha vitandani mwao. Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao na panga mbili zenye makali mkononi mwao kutekeleza kisasi juu ya mataifa na matendo ya adhabu juu ya watu. Nao watawafunga wafalme wao kwa minyororo na wakuu wao kwa pingu za chuma. Watatekeleza hukumu ambayo imeandikwa. Hii itakuwa ni heshima kwa ajili ya watakatifu wake wote. Msifuni Yahwe.