150
Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake. Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake. Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi. Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi. Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana. Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe.