46
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya mwana wa Korah; seti kwenye Alamoth. Wimbo. Mungu kwetu ni kimbilio la usalama na nguvu, upatikanao tele wakati wa mateso. Hivyo hatutaogopa, hata kama dunia italazimika kubadilika, hata kama milima italazimika kutetemeka na kuangukia kwenye mtima wa bahari, hata kama maji yatavuma kwa kishindo kikuu, hata kama milima itatetemeka kwa vurugu ya maji. Selah Kuna mto, mikondo yake huufanya mji wa Mungu kufurahi, mahali patakatifu pa hema ya Aliye Juu. Mungu yuko katikati yake; naye hatasogezwa; Mungu atamsaidia, naye atafanya hivyo asubuhi na mapema. Mataifa yalikasirika na falme zikataharuki; yeye alipaza sauti yake, na nchi ikayeyuka. Yahwe wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Selah Njoni, mtazame matendo ya Yahwe, uharibifu alioufanya juu ya nchi. Anaisitisha vita kwenye nchi; yeye anauvunja upinde na kuikata vipande vipande mishale; anazichoma ngao. 10 Mkae kimya na mjue kuwa mimi ni Mungu; nitainuliwa juu ya nchi. 11 Mungu wa majeshi yuko pamoja nasi; Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu la usalama. Serah