47
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah. Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi. Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote. Yeye anawatiisha chini yetu na mataifa chini ya miguu yetu. Yeye huchagua urithi kwa ajili yetu, utukufu wa Yakobo ambaye alimpenda. Serah Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu. Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa. Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi. Wakuu wa watu wamekusanyika pamoja kwa watu wa Mungu wa Ibrahimu; kwa kuwa ngao za duniani ni za Mungu; yeye ameinuliwa juu sana.