57
Kwa kiongozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi; wakati alipo mkimbia Sauli, pangoni. Unihurumie, Mungu, unihurumie mimi, kwa maana ninakukimbilia wewe mpaka matatizo haya yaishe. Ninakaa chini ya mbawa za zako kwa ajili ya ulinzi mpaka huu uharibifu utakapoisha. Nitakulilia Mungu uliye hai, kwa Mungu, afanyaye mambo yote kwa ajili yangu. Yeye atatuma msaada kutoka mbinguni na kuniokoa, ana hasira na wale wanaonishambulia. Selah Mungu atanitumia upendo wake mwema na uaminifu wake. Uhai wangu uko katikati ya simba; niko katikati ya wale walio tayari kunila. Niko katikati ya watu ambao meno yao ni mikuki na mishale, na ambao ndimi zao ni kali kama upanga. Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu, utukufu wako uwe juu ya nchi yote. Wao walisambaza nje wavu kwa ajili ya miguu yangu; nilikuwa na shida sana. Walichimba shimo mbele yangu. Wao wenyewe wameangukia katikati ya shimo! Selah Moyo wangu umeponywa, Mungu, moyo wangu umeponywa, nitaimba, ndiyo, nitaimba sifa. Inuka, moyo wa thamani; inuka, kinanda na kinubi; nitaamka alfajiri. Nitakushukuru wewe, Bwana, kati ya watu; Kati ya mataifa nitakuimbia sifa. 10 Maana upendo wako usiokwisha, huzifikia mbingu; na uaminifu wako mawinguni. 11 Uinuliwe, Mungu, juu ya mbingu; na utukufu wako uinuliwe juu ya nchi yote.