58
Kwa kiongiozi wa muziki; seti kwenye Al Tashheth. Zaburi ya Daudi. Zaburi. Je, ninyi watawala mnaongea haki? Mnahukumu kwa haki, ninyi watu? Hapana, mnafanya uovu mioyoni mwenu; munaeneza vurugu nchi yote kwa mikono yenu. Waovu huenenda katika upotovu hata walipokuwa tumboni; wao wanaenenda katika upotovu tangu kuzaliwa, wakiongea uongo. Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake, ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao. Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe. Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha. Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua. Kabla ya vyungu vyenu kupata joto la kuungua kwa miiba, yeye ataviondosha kwa upepo mkali, miiba ya kijani yote na ile inayoungua. 10 Mwenye haki atafurahia atakapoona kisasi cha Mungu; ataiosha miguu yake kwenye damu ya waovu, 11 hivyo watu watasema, “Hakika kuna tuzo kwa ajili ya mtu wenye haki; hakika kuna Mungu ahukumuye ulimwengu.”