6
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi, weka kwenye mtindo wa Sheminith. Zaburi ya Daudi. Yahweh, usinikemee ukiwa na hasira au usiniadhibu katika gadhabu yako. Unihurumie, Yahwe, kwa maana ni dhaifu; uniponye, Yahweh, kwa kuwa mifupa yangu ina tikisika. Moyo wangu pia umesumbuka sana. Lakini wewe, Yahweh, mpaka lini hali hii itaendelea? Rudi, Yahweh! uniokoe. Uniokoe kwa sababu ya uaminifu wa agano lako! kwa kuwa kifoni hakuna kumbukumbu lako. Kuzimuni ni nani atakaye kushukuru? Nimechoshwa na kuugua kwangu. Ninalowanisha kitanda changu kwa machozi usiku kucha; ninaosha kiti changu kwa machozi. Macho yangu yanafifia kwa kulia sana; yanazidi kuwa dhaifu kwa sababu ya adaui zangu. Ondokeni kwangu, nyote mtendao maovu; kwa kuwa Yahweh amesikia sauti ya kilio changu. Yahweh amesikia malalamiko yangu kwa ajili ya huruma; Yahweh ameyapokea maombi yangu. 10 Maadui zangu wote wataaibishwa na kuteswa sana. Watarudi nyuma na ghafra kufedheheshwa.