63
Zaburi ya Daudi, wakati yeye alipokuwa katika jangwa la Yuda. Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji. Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako. Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe. Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu. Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe, nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku. Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia. Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia. Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi; 10 watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha. 11 Bali mfalme atashangilia katika Mungu; yeyote anaye apa kupitia yeye atajivunia yeye, lakini vinywa ya wale wasemao uongo watanyamazishwa.