67
Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. zaburi, wimbo. Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye.