70
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; kuleta kumbukumbu. Uniokoe, Mungu! Yahwe, njoo haraka na unisaidie mimi. Wale wajaribuo kuchukua uhai wangu waaibishwe na kufedheheshwa; warudishwe nyuma na wasiheshimiwe, wale wafurahiao katika maumivu yangu. Warudishwe nyuma kwa sababu ya aibu yao, wale wasemao, “Aha, aha.” Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu asifiwe.” Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.