89
Zaburi ya Ethan Muezrahite.
1 Nitimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele. Nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo.
2 Maana nimesema, “Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni.”
3 “Nimefanya agano na wateule wangu, nimeapa kiapo kwa Daudi mtumishi wangu.
4 Nitauimarisha uzao wako milele, na nitauimarisha utawala wako vizazi vyote.” Selah
5 Mbingu husifu maajabu yako, Yahwe; kweli yako inasifiwa katika kusanyiko la watakatifu.
6 Maana ni nani katika mbingu aweza kulinganishwa na Yahwe? Ambaye kati ya wana wa miungu ni kama Yahwe?
7 Ni Mungu anaye heshimiwa sana katika baraza la watakatifu naye ni wakutisha kati ya wote wanao mzunguka.
8 Yahwe, Mungu wa majeshi, ni nani aliye na nguvu kama wewe, Yahwe? Kweli yako inakuzunguka.
9 Wewe huitawala bahari yenye nguvu; mawimbi yainukapo, wewe huyatuliza.
10 Ulimwangamiza Rahabu kama mmoja aliye uliwa. Uliwatawanya adui zako kwa mkono wako wenye nguvu.
11 Mbingu ni zako wewe, na nchi pia. Uliiumba dunia na vyote vilivyomo.
12 Uliumba kaskazini na kusini. Tabori na Hermoni hulifurahia jina lako.
13 una mkono wa uweza na mkono wenye nguvu, na mkono wako wa kuume uko juu.
14 Haki na hukumu ni msingi wa kiti chako. Uaminifu wa agano lako na uaminifu huja mbele zako.
15 Wamebarikiwa watu wakuabuduo wewe! Yahwe, wanatembea katika nuru ya uso wako.
16 Siku zote wanafurahia katika jina lako, na katika haki yako wanakutukuza wewe.
17 Wewe ni fahari ya nguvu zao, na kwa nguvu zako tu washindi.
18 Maana ngao zetu ni za kwako Yahwe; mfalme wetu ni wa Mtakatifu wa Israeli.
19 Muda mrefu uliopita ulizungumza na waaminfu wako katika maono; ulisema, “Nimeweka taji juu ya mwenye nguvu; nimemuinua aliyechaguliwa kutoka kati ya watu.
20 Nimemchagua Daudi mtumishi wangu; kwa mafuta yangu matakatifu nimempaka yeye.
21 Mkono wangu utamsaidia yeye; mkono wangu utamtia nguvu.
22 Hakuna adui atakaye mdanganya; hakuna mwana wa uovu atakaye muonea.
23 Nitawaangamiza adui zake mbele yake; nitawaua wale wamchukiao.
24 Kweli yangu na uaminifu wa agano vitakuwa pamoja naye; kupitia jina langu atakuwa mshindi.
25 Nitaweka mkono wake juu ya bahari na mkono wake wa kuume juu ya mito.
26 Yeye ataniita, 'Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, na mwamba wa wokovu wangu.'
27 Nitamjalia kuwa kama mzaliwa wangu wa kwanza, aliye inuliwa zaidi juu ya wafalme wa nchi.
28 Nitaongeza uaminifu wa agano langu kwake milele; na agano langu pamoja naye litakuwa salama.
29 Nitaufanya uzao wake kudumu milele na kiti chake cha enzi kitadumu kama mbingu zilizo juu.
30 Ikiwa watoto wake wataziacha sheria zangu na kutokutii amri zangu,
31 na kama watazivunja sheria zangu na kutokuzishika amri zangu,
32 ndipo nitauadhiu uasi wao kwa fimbo na uovu wao kwa makofi.
33 Lakini sitauondoa kwake upendo wangu thabiti wala kutokuwa mwaminifu kwa ahadi yangu.
34 Sitavunja agano langu wala kubadilisha maneno ya midomoni mwangu.
35 Mara moja na kwa yote, nimeapa kwa utakatifu wangu sitamdanganya Daudi:
36 uzao wake utaendelea milele na kiti chake cha enzi kama vile jua mbele yangu.
37 Kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu mawinguni.” Selah
38 Lakini wewe umemtupa na kumkataa; umemkasirikia mfalme mpakwa mafuta wako.
39 Wewe umelikataa agano la mtumishi wako. Umeinajisi taji yake ardhini.
40 Umevunja kuta zake zote. Umeharibu ngome yake.
41 Wapita njia wote wamemuibia, amekuwa kitu chenye kinyaa kwa majirani zake.
42 Umeinua mkono wa kuume wa adui zake; umewafurahisha adui zake wote.
43 Umeyageuza makali ya upanga wake. Na hukumfanya asimame awapo vitani.
44 Umeimaliza fahari yake; umekitupa ardhini kiti chake cha enzi.
45 Umefupisha siku za ujana wake. Umemfunika kwa aibu. Selah
46 Mpaka lini, Yahwe? utajificha, milele? Mpaka lini hasira yako itawaka kama moto?
47 Oh, fikiria jinsi muda wangu ulivyo mfupi, na ni kwa ajili gani umewaumba wana wote wa wanadamu wasio na manufaa!
48 Ni nani aweza kuishi na asife, au atakaye iokoa nafsi yake dhidi ya mkono wa kuzimu? Selah
49 Bwana, yako wapi matendo yako ya zamani ya uaminifu wa agano ambayo ulimwapia Daudi katika kweli yako?
50 Kumbuka, Bwana, watumishi wako walivyodhihakiwa na vile nilivyo vumilia moyoni mwangu matusi mengi dhidi ya mataifa.
51 Maadui zako wanavurumiza matusi, Yahwe; wanadhihaki nyayo za mpakwa mafuta wako.
52 Atukuzwe Yahwe milele. Amina na Amina. Kitabu cha Nne