29
1 Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.
2 Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.
3 Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, katika mwezi wa kwanza, Hezekia aliifungua milango ya nyumba ya Yahwe na kuikarabati.
4 Akawaleta ndani makuhani na Walawi, na akawakusanya pamoaja katika uwanda upande wa mashariki.
5 Akawaambia, “Nisikilizeni, ninyi Walawi! Jitakaseni wenyewe, na itakaseni nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zenu, na uondoeni mbali uchafu kutoka kwenye sehemu takatifu.
6 Kwa kuwa babu zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macaho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutoka sehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao.
7 Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.
8 Kwa hiyo hasira ya Yahwe ilikuwa imeshuka juu ya Yuda na Yerusalemu, na amewafanya kuwa kitu cha wasiwasi, cha hofu, na cha kudharauriwa, kama mnavyoona kwa macho yenu.
9 Hii ndiyo maana mababu zetu wameanguka kwa upanga, na wana wetu, binti zetu, na wake zetu wako katika utumwa kwa sababu ya hili.
10 Sasa ni katika moyo wangu kufanya agano na Yahwe, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali iweze kugeukia mbali nasi.
11 Wanangu, msiwe wavivu sas, kwa kuwa Yahwe amewachagua kwa ajili ya kusimama mbe yake, kwa ajili ya kumwabudu yeye, na kwamba muwe watumishi wake na kufukiza uvumba.”
12 Basi Walawi wakainuka; Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa watu wa Kohathi; na wa watu wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wargeshoni, Yoa mwana wa Zimna, na Edeni mwana wa Yoa;
13 wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;
14 wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.
15 Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe.
16 Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwnye kijito cha Kidroni.
17 Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza.
18 Kisha wakaenda kwa Hezekia, mfalme, ndani ya ikulu na kusema, “Tumeisafisha nyumba yote ya Yahwe, madhabahu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa pamoja na vifaa vyake vyote, na meza ya mkate wa uwepo, pamoja na vifaa vyake vyote.
19 Kwa hiyo tumejiandaa na tumevitakasa vitu vyote ambavyo Mfalme Ahazi aliviondoa wakati alipoenda kwa ukengeufu katika kipindi cha utawala wake, ona, viko mbele ya madhabahu ya Yahwe.”
20 Kisha Hezekia mfalme akaamka mapema asubuhi na kuwakusanya viongozi wa miji; akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.
21 Wakaleta ng'ombe waume saba, kondoo waume saba, wanakondoo saba, mbuzi waume saba kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya mfalme, kwa ajili ya patakatifu, kwa ajili ya Yuda. Akawaamuru makuhani, wana wa Haruni, kuwatoa sadaka juu ya madhabahu ya Yahwe.
22 Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu.
23 Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadka ya dhambi mbele ya mfalme na kusnyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi.
24 Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.
25 Hezekia akawaweka Walawi katika nyumba ya Yahwe wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, akiwapanga kwa amri ya Daaudi, Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani, nabii, kwa maana amri ilitoka kwa Yahwe kupitia manabii wake.
26 Walawi wakasimama na vyombo vya Daudi, na makauhani wakasimama na matarumbeta.
27 Hezekia akawaamuru kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Sadaka zilipoanza, wimbo wa Yahwe ukaanza pia, kwa matarumbeta, pamoja na vyombo vya Daudi, mfalme wa Israeli.
28 Kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, na wapiga matarumbeta wakapiga; yote hayo yakaendele hadi sadaka za kuteketezwa zilizipokwisha.
29 Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na watu waliokuwepo pamoja naye wakainama, na kusujudu.
30 Vile vile, Hezekia, mfalme, na viongozi wakawaamuru Walawi kuimba ili kumsifu Yahwe kwa maneno ya Daudi na ya Asafu, mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama chini wakasujudu.
31 Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe. Njoni hapa na mlete sadaka na dhabihu za shukrani katika nyumba ya Yahwe.” Kusanyiko wakaleta sadka na dhabihu za shukrani, na wote waliaokuwa na moyo wa kuhiyalika wakaleta sadka za kuteketezwa.
32 Hesabu ya sadaka za kuteketezwa ambazo kusanyiko walileta ilikuwa ng'ombe sabini, kondoo waume mia moja, na wanakondo waume mia mbili. Wote hao walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe.
33 Sadaka za kuwekwa wakfu zilikuwa ng'ome mia sita na kondoo elfu tatu.
34 Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuchuna sadaka zote za kuteketezwa, kwa hiyo ndgugu zao, Walawi, wakawasaidia hadi kazi ilipoisha, na hadi makuhani walipoweza kujitakasa wenyewe, kwa maana Walawi walikuwa makaini sana kujitaksa wenyewe kuliko makuhani.
35 Zaidi ya hayo, palikuwa na sadaka za kuteketezwa nyingi sana; zilitolewa pamoja na sadaka za mafauta za amani, na kulikuwa na sadaka za vinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo huduma ya nyumba ya Yahwe ikawekwa katika utaratibu.
36 Hezekia akafurahia, na watu pia, kwa sababu ya kile ambacho Mungu alikuwa ameandaa kwa ajili ya watu, kwa maana kazi ilikuwa imekamilika haraka.