100
Zaburi ya shukrani. Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote. Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha. Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake. Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.