122
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu, wa Daudi. Nilifurahi waliponiambia, “Na twende kwenye Nyumba ya Yahwe.” Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama ndani ya malango yako! Ee Yerusalemu, uliojengwa kama mji uliopangiliwa kwa umakini! Makabila huenda juu Yerusalemu, makabila ya Yahwe; kama ushuhuda wa Israeli, kulishukuru jina la Yahwe. Huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya nyumba ya Daudi. Ombeni kwa ajili ya amani ya Yerusalemu! “Wote wakupendao wawe na amani. Amani iwepo ndani ya kuta zako ili ikutetee, na wawe na amani ndani ya ngome zako.” Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu nitasema, “Amani iwe ndani yenu.” Kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu, nitatafuta mema kwa ajili yako.