123
Wimbo wa kwenda hekaluni kuabudu. Nakuinulia macho yangu, wewe uketiye mbinguni. Tazama, kama vile macho ya watumishi watazamapo kwenye mkono wa Bwana wao, na kama macho ya mjakazi yatazamapo mkono wa bibi yake, ndivyo hivyo macho yetu yanamtazama Yahwe mpaka atakapo tuhurumia. Ee Yahwe, utuhurumie, kwa maana tunadhalilishwa sana. Tumeshibishwa mzaha wa wenye kiburi na dharau ya wenye majivuno.