124
Wimbo wa kwenda kuabudu; wa Daudi. “Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa, “Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu, basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu. Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia. Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.” Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao. Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka. Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.