91
1 Yeye aishiye katika makazi ya Aliye Juu atakaa katika uvuli wa mwenyezi.
2 Nami nitasema kuhusu Yahwe, “Yeye ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye niaamini katika yeye.”
3 Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti.
4 Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi.
5 Nawe hautaogopeshwa na vitisho wakati wa usiku, wala mishale ipaayo kwa siku,
6 wala pigo lizungukalo gizani, wala ugonjwa ujao wakati wa mchana.
7 Maelfu waweza kuangukia upande wako na makumi elfu mkono wako wa kuume, lakini uovu hauwezi kukupata.
8 Wewe utatazama tu na kuona hukumu ya waovu.
9 Kwa kuwa Yahwe ni kimbilio langu! Umfanye Aliye Juu kuwa kimbilio lako pia.
10 Hakuna uovu utakao kushinda wewe; mateso hayatakuja karibu na nyumba yako.
11 Maana yeye atawaelekeza malaika moja kwa moja kukulinda wewe, na kukuwekea ulinzi katika njia zako zote.
12 Nao watakuinua juu kwa mikono yao ili usiweze kujigonga mguu wako kwenye jiwe.
13 Utawaangamiza simba na nyoka chini ya miguu yako; utawakanyaga wana-simba na nyoka.
14 Kwa sababu amejitoa kwangu, nitamuokoa. Nitamlinda kwa sababu yeye ni mwaminifu kwangu.
15 Aniitapo, nitamjibu. Katika shida nitakuwa naye; nitampatia ushindi na nitamuheshimu.
16 Nitamtosheleza kwa maisha malefu na kumuonesha wokovu wangu.