92
Zaburi, wimbo kwa ajili ya siku ya Sabato. Ni jambo jema kumshukuru Yahwe na kuliimbia sifa jina lako, Uliye Juu, kutangaza uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi na uaminifu wako kila usiku, kwa kinubi cha nyuzi kumi na kwa tuni ya kinubi. Kwa kuwa wewe, Yahwe, matendo yako yamenifurahisha. Nitaimba kwa furaha kwa sababu ya matendo ya mikono yako. Ni jinsi gani matendo yako ni makuu, Yahwe! mawazo yako ni ya kina. Mtu mpumbavu hawezi kuyajua, wala mjinga kuyaelewa haya: Wasio haki watakapochipuka kama nyasi, na hata watendao uovu watakapo stawi, bado wataangamizwa kwenye uharibifu wa milele. Lakini wewe, Yahwe, utatawala milele. Hakika, watazame adui zako, Yahwe! Hakika, watazame adui zako. Wataangamia! Wale wote watendao maovu watatawanywa. 10 Wewe umeyainua mapembe yangu kama mapembe ya Nyati wa porini; nimepakwa mafuta safi. 11 Macho yangu yameona kuanguka kwa adui zangu; masikio yangu yamesikia maangamizi ya maadui zangu waovu. 12 Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni. 13 Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe; wakistawi katika nyua za Mungu wetu. 14 Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya, 15 kutangaza kuwa Yahwe ni wa haki. Yeye ni mwamba wangu, na hakuna udhalimu ndani yake.