93
Yahwe anatawala; amevikwa adhama; Yahwe amejivika na kujifunga nguvu. Ulimwengu umeimalishwa; hauwezi kusogezwa. Kiti chako cha enzi kimeimarishwa nyakati za kale; umekuwepo siku zote. Bahari zimeinuka, Yahwe; zimemepaza sauti zao; mawimbi ya bahari yapiga ghasia na ngurumo. Zaidi ya ghasia ya mawimbi mengi, mawimbi ya bahari yenye nguvu, Yahwe aliye juu ni mwenye nguvu. Amri zako makini ni za kuaminika sana; utakatifu huipamba nyumba yako, Yahwe, milele.